Bwana mmoja aliyeishi katika nchi moja maarufu sana aliwahi kusikia kuwa hakipo kitu chenye utamu kifani cha asali. Watu wengi waliozuru nchi ya Tanzania na kurejea Kenya, walimhadithia kuhusu utamu wa asali. Kwamba halua kando. Alitaka amwombe mmoja amletee asali hiyo lakini hakupenda kufanyiwa mambo. Alitaka aone ndipo aambe bali asiambiwe tu. Sifa hizi za utamu wa asali zilimchochea hadi naye akapanga safari ya kwenda Tanzania kujionea hayo na kuonja. Aliambiwa kuwa asali hutengenezwa na wadudu fulani wenye kelele ila wakali kuliko simba. Alitaka kuwaona wadudu hawa wanaotumia malighafi hasi kutengeneza asali tamu.
Alifika katika nchi hiyo ya jirani na kupelekwa hadi katika mbuga ya wanyama. Wahudumu wa mbuga hiyo walinuia kumpeleka hadi kwenye magenge ambamo nyuki waliishi. Njiani mtu huyo aliisikia sauti ya wadudu. Kwa kuwa alikuwa na uchu, alikimbia hadi kule ilikotokea. Alifika walikokuwa wadudu hao. Kwenye mzoga ndiko wadudu hao walikokuwa wakifanyia kelele. "hawa ndiyo nyuki wa asali tamu?" aliwauliza wahudu. "hapana." alijibiwa na mhudumu mmoja. "lakini niliambiwa nyuki wa asali tamu hufanya kelele na hutumia malighafi machafu ili kutengeneza asali tamu. Nauona hapa mzoga uliooza na wadudu wenye kelele wakusanyika pale. Haikosi wawe hao hao nyuki." "la, umesahau jambo moja, " mhudumu mmoja alisema, "nyuki uliambiwa ni wakali. Ndiyo, hawa wana kelele na pia malighafi yao ni uchafu, lakini umemwona moja akikung'ata? Hawa ni nzi babu we'"
Waliingia ndani hadi magengeni. Loh! Alikaribishwa kwa kelele. Akaongozwa hadi nyuki walikotengenezea asali. Akapenda. Wapo waliozunguka kwa kelele na kung'ata adui na wapo waliofanya kazi ya kugema bila kelele. Akavuta taswira ya wale nzi. Akabaini tofauti yao na hawa nyuki. Alipoambiwa aonje asali tamu, alikataa. Alidai kuwa asali tamu ni ile ya kuleta mabadiliko licha kuwapo ugumu katika mazingira. Aliapa kurudi kenya mara moja ili kuwaambia wenzao tofauti kati ya NYUKI na NZI. Kumbe ukiwa na makeke na utulie, waweza kujenga ghorofa kwenye mazingira yoyote yale. Lakini kwao Kenya, wengi ni wa kelele na papara 'hali wa' kwenye mzoga unaonuka. Hawajali. Akifika labda, atawafunza wenzake jinsi ya kufanya kelele za kufaidi wakati ukifika. Labda atawatuliza na kuona ikiwa kuna nyuki ambao watatengeneza asali tamu katika nchi yao hasa msimu huu ambapo uchafu umehanikiza. ASALI TAMU

No comments:
Post a Comment