Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Saturday, 20 October 2018

MASHUJAA WETU




MASHUJAA WETU
Wakati umewadia, mashujaa kutambua,
Shairi nawandikia, siseme nawasumbua,
Sikiliza nawambia, nafasi nimechukua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka,

Alisifika bondia, watu wengi wamjua,
Nchi alipigania, na kuipa vitumbua,
Conje' ninakusifia, masumbwi ulifufua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka

Oliechi nawe pia, sifazo ninazizua,
Uwanjani likuchia, malango ukifungua,
Nchi ulisaidia, Afukoni kuzumbua
Shujaa ulesifika, kwa Shairi nakusuka

Mulee nawatajia, vipaji uligundua,
Ndasaba nashadidia, nyavu ulisukutua,
Napunyi yule bondia, wapinzani lilipua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka.
@Tungo za Daniel kaka Si'wa
Fb @Kaka Si'wa


No comments:

Post a Comment