Wametugeuza nzi, matatizo hawaoni
Wasokuwa na mapenzi,mwatuona hawayawani
Hawasikii ukwenzi, wana nta sikioni
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Habari magazetini, wajifanya hawasomi
Na picha mitandaoni, hawaoni asilani
Matangazo redioni, hawajui zasemani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Kila siku vikaoni, waketi wakijadili
Na vinyuaji mezani, wakikagua faili
Wanapofika mwishoni, midia hawaikabili
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Maji yakikosekana, kwao hilo hawajali
Watasimama bayana, wakitenga hela kweli
Hatimaye wanakana, na kuilaani hali
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Njaa inapovamiza, nchi kule kaskazi
Wajifanya wanakaza, sura bandia za kazi
Vilio wanavipaza, na hawatoi machozi
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Wananchi wakilia, turkana na Baringo
Ufisadi watwambia, kugeuza zetu shingo
Lao ni kututania, wakideka kwa maringo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Na vyakula magalani, vinaoza twaambiwa
Nazo hela mabenkini, zinazidi kuibiwa
Na mnyonge masikini, kwa njaa anauliwa
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Mirefu yao midomo, hawaishi majigambo
Mwetu shida zilizomo, waziona vijimambo
Waiba bila ukomo, wakiboboja umombo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Matozi yamenitoka, yamenilovya machoni
Nazo nguvu zanitoka, kwa ulodumu uhuni
Kaka Si'wa naodoka, nikikemea shetwani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Wasokuwa na mapenzi,mwatuona hawayawani
Hawasikii ukwenzi, wana nta sikioni
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Habari magazetini, wajifanya hawasomi
Na picha mitandaoni, hawaoni asilani
Matangazo redioni, hawajui zasemani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Kila siku vikaoni, waketi wakijadili
Na vinyuaji mezani, wakikagua faili
Wanapofika mwishoni, midia hawaikabili
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Maji yakikosekana, kwao hilo hawajali
Watasimama bayana, wakitenga hela kweli
Hatimaye wanakana, na kuilaani hali
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Njaa inapovamiza, nchi kule kaskazi
Wajifanya wanakaza, sura bandia za kazi
Vilio wanavipaza, na hawatoi machozi
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Wananchi wakilia, turkana na Baringo
Ufisadi watwambia, kugeuza zetu shingo
Lao ni kututania, wakideka kwa maringo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Na vyakula magalani, vinaoza twaambiwa
Nazo hela mabenkini, zinazidi kuibiwa
Na mnyonge masikini, kwa njaa anauliwa
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Mirefu yao midomo, hawaishi majigambo
Mwetu shida zilizomo, waziona vijimambo
Waiba bila ukomo, wakiboboja umombo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera
Matozi yamenitoka, yamenilovya machoni
Nazo nguvu zanitoka, kwa ulodumu uhuni
Kaka Si'wa naodoka, nikikemea shetwani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

No comments:
Post a Comment