Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Tuesday, 25 March 2025

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufisadi gavana huyo ayehudumia muhula wake wa mwisho kama gavana. Lusaka amekashifiwa kwa hatua yake ya kufutilia mbali mpango wa scholarship ulianzishwa na mtangulizi wake Wafula Wangamati. Miongoni mwa maovu anayodaiwa kutekeleza katika hatamu yake hii ya mwisho ni pamoja na :

Barabara duni

Hali mbaya katika zahanati nyingi kwenye eneo gatuzi la Bungoma.

Ufisadi uliokithiri

Lusaka amekumbushwa kuhusu kashifa ya bero "Wheelbarrow" iliyomwandamwa katika awamu yake ya awali, wengi wakimtaja kuwa Tatizo sugu ambalo lililimbikiziwa watu wa Bungoma na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula. Haya hapa baadhi ya maoni ya watu.

Kevin Zimiu "Governor umesahau wheelbarrow scandalπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ mimi sioni maendeleo as ni kama ulikam ukule chenye ulipakisha. Major ako sawa omukosi"

Patrick Namaswa "Mheshimiwa, oli ukaamua kulima yeye likuma liemungoro yitaa ?

But truth be told, why are you defending yourself? 

Can you look straight into the eyes of an ecde trained teacher and tell him or her that your county exist in terms offering employment?

A farmer and tell them you really care?

Dispensaries and say you exist?

Roads and say you're the father of th


e county, water, this is just to mention but a few. Enywe ta wase!"

Caroline Chazima " This man's first development move was to remove all students who his predecessor had made beneficiaries of the county education scholarship scheme.dies he think the parents and students who were wounded by him clap their hands when engages with his colleague.Lisaka, you have let us down Which road do you use from Bungoma to kamukuywa,from bgm to kamukuywa through webuye or chwele Kimilili.Ever imagined the trauma the pple along Kimilili,khachonge are going through.Lusaka,we need tangible change.."

Chris Wekesa " You're the mistake wetangula did to Bungoma. Honestly is there any tangible thing you can show since you assumed office. Waluke has spoken my mind. you silenced senator wakoli when he claims about 25 million squandered during beautification of Bungoma town. You're a true description of corruption. I thank waluke for standing in as a senator"

Mukeni Mukeni "When it comes to theft sorry sir we don't have respect and decoram what we want is accountability & transparent to the people of bungoma. Kanduyi stadium 🏟️ is being funded by national government" 

Suez Sindani "Wanaitaga wateva calling the kettle or sufuria black,so absurd,bring a screenshot of how you bought a wheel barrow @109,000 you're all corrupt" 



Friday, 3 January 2025

IF BABUKUSU AREN'T BEWITCHED...!!

Bali koo!! Mbakarira mufubi ali ese olimukhusia, khane olimukhusia ali anyuma - He who hurries for an orphan does not raise him, because the one who will raise him comes later. Unfortunately we cheered when the one who is showing signs to raise is stripped naked. 

 


My people were once and are still being referred to as Siyanja barende - the lover of foreigners. I was always against the proverb but what happened during the funeral of Mama Annah Nanyama, the Mother to Speaker Moses Wetangula proved me wrong. Of course Kenyans know that there's a big rift ideologically between Speaker Wetangula and Governor Natembea, but it wasn't prudent for Babukusu to jeer their own son when he stood to speak in the funeral. Governor condemned the politics of blackmail and mbekho mbekho from our Mps especially in funerals yet they publicly claim to be in government and have forums to push for the community's agenda. He spoke against the perceived abductions. His words were factual. 

It was discouraging when Babukusu from Bungoma cheered on when Kimani Ichungwa lectured their son in public. It was sad when they responded with vigour and vehemence when the majority leader, coming from far away painted blood on the hands and face of their son. Can a son, a daughter, a brother, a sister not only watch but cheer and laugh when their father, son or brother is stripped naked by omurende? Something must be wrong with us! What a shame!!! Just a little reminder to us, Mao wo wasio sakhusinga wanoka ta- your colleague's mother cannot wash you clean. 

Tuesday, 19 March 2019

MABALOZI WA SERA

Wametugeuza nzi, matatizo hawaoni
Wasokuwa na mapenzi,mwatuona hawayawani
Hawasikii ukwenzi, wana nta sikioni
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Habari magazetini, wajifanya hawasomi
Na picha mitandaoni, hawaoni asilani
Matangazo redioni, hawajui zasemani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Kila siku vikaoni, waketi wakijadili
Na vinyuaji mezani, wakikagua faili
Wanapofika mwishoni, midia hawaikabili
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Maji yakikosekana, kwao hilo hawajali
Watasimama bayana, wakitenga hela kweli
Hatimaye wanakana, na kuilaani hali
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Njaa inapovamiza, nchi kule kaskazi
Wajifanya wanakaza, sura bandia za kazi
Vilio wanavipaza, na hawatoi machozi
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Wananchi wakilia, turkana na Baringo
Ufisadi watwambia, kugeuza zetu shingo
Lao ni kututania, wakideka kwa maringo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Na vyakula magalani, vinaoza twaambiwa
Nazo hela mabenkini, zinazidi kuibiwa
Na mnyonge masikini, kwa njaa anauliwa
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Mirefu yao midomo, hawaishi majigambo
Mwetu shida zilizomo, waziona vijimambo
Waiba bila ukomo, wakiboboja umombo
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera

Matozi yamenitoka, yamenilovya machoni
Nazo nguvu zanitoka, kwa ulodumu uhuni
Kaka Si'wa naodoka, nikikemea shetwani
Mabalozi wake sera, wamezika zao sera




Sunday, 6 January 2019

SIYATAKI MAPENZI

Sitaki tena kupenda
Ninakimbia nanenda
Nimeshindwa udifenda
Sivumilii ninakwenda

Mapenzi yamenisibu
Ndwele iso matibabu
Menisaliti muhibu
Amerarua kitabu

Kwa hali lijitolea
Makubwa kamtendea
Mabaya meninenea
Nakwenda natokomea

Majonzi linizidia
Usiku lijililia
Penzi lochangamkia
Kwa sasa lanichukia

Mwenyezi nihurumie
Machungu nipunguzie
Siniache nijililie
Nishike sijifilie

Saturday, 20 October 2018

MASHUJAA WETU




MASHUJAA WETU
Wakati umewadia, mashujaa kutambua,
Shairi nawandikia, siseme nawasumbua,
Sikiliza nawambia, nafasi nimechukua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka,

Alisifika bondia, watu wengi wamjua,
Nchi alipigania, na kuipa vitumbua,
Conje' ninakusifia, masumbwi ulifufua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka

Oliechi nawe pia, sifazo ninazizua,
Uwanjani likuchia, malango ukifungua,
Nchi ulisaidia, Afukoni kuzumbua
Shujaa ulesifika, kwa Shairi nakusuka

Mulee nawatajia, vipaji uligundua,
Ndasaba nashadidia, nyavu ulisukutua,
Napunyi yule bondia, wapinzani lilipua,
Shujaa ulesifika, kwa shairi nakusuka.
@Tungo za Daniel kaka Si'wa
Fb @Kaka Si'wa


Friday, 28 September 2018

Luuya poem : KAMAKHUWA KE 'BAAPENI.

Baamenywa be' Bungoma,
Neende eenyenywe baluya,
Rekeresia kamkhuwa,
Kakama muno mukhanwa,
Kamakhuwa khubapeni

Baapeni be' ebuluya,
Khuulilaanga nomwimba,
Chinyimbo chenywe chaanula,
Mukilaanga kumwoyo kwetikitia,
Kamkhuwa ke' baapeni!

Baapeni nomwimba kimyenya,
Imba nowenya khusomya,
Akhemba sa khukhwebonia,
Namwe ta' khukhwefumia,
Kamakhuwa ke' baapeni!

Baapeni khemukhebusia,
Wasike wa Musungu kembanga,
Kalolomalomakho mu' kechingoba,
Akhaata nende khuruunda,
Kamakhuwa kebaapeni!

Baapeni nomusima,
Khukheebusie niyo khwama,
Nyo 'mbo khumanye niyo khucha,
Ao sibukusu silafuma,
Kamkhuwa ke' baapeni...

Lelo baapeni muukia,
Mwimba sa oli mukhana!
Mwimba babaami khubafumia,
Nyo 'mbo munyole lipesa,
Kamakhuwa ke' baapeni!

Baapeni lundi mutiiba!
Lipesa onamala wanyola,
Khumela sofuchikha ta,
Bisonga otikitia namwe otikitia!
Kamakhuwa ke' baapeni!

 @NAASIMA SIBUKUSU,
@ Daniel kaka Si'wa.

,

Saturday, 8 September 2018

HEKO HARAMBEE STARS

Bahari ilo shwari, hi'toa mwanamaji stadi,
Mmeyapitia yalo mengi, lipokuwa safarini,
Majeraha ya wachezaji, yaliwapa wasiwasi,
Heko harambee stars, mmechuna miamba,

Mlimkosa wanyama, Mariga na Masika,
Vifyefye wakamuona, dharau ikahanikiza,
Fimbo mmewachapa, chooni watalilia,
Heko Harambee Stars, mmetupa furaha ,

Mmefua tumaini, la kufuzu mwakani,
Mmerejea meelini, hadi ng'ambo kusafiri,
Heri twawatakieni, kwa yote ya mbeleni,
Heko Harambee stars, meondoa jinamizini,

Mashabiki walojima, uwanjani kujituma,
Sauti zao lihanikiza, ili moyo kuwapatia,
Sitakuwa mkiritimba, pongezi kuwanyima,
Heko Harambee Stars, mmepaa nguuni.

Nawarai wasimamizi, wizara na serikali,
Mjitume kila hali, kushajiisha wachezaji,
Mzitenge fulusi, kufadhili na kuzawidi,
Heko Harambee stars, ushindi umetufaa.

Tamati ninapotua, wakenya na Afrika,
Muondokeni ulaya, mrejee kwenye bara,
Vilabu vyetu shangilia, mchezo kuukuza,
Heko Harambee Stars, macho metufungua.

@Tungo za Daniel kaka Si'wa
Nasaka - Bungoma
0725727519