Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Sunday, 26 June 2016

MWALO REMMY

                  MWALO REMMY
Wa tatu ni mwaka wake,Moi ndicho chuo chake,
Bungoma kaunti yake, alikozaliwa yeye,
Magharibi 'neo lake, Mkenya kabila lake,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

Nakumbuka alifiwa, ila hakutetereka,
Namtakia makiwa, asije kapepesuka,
Namuombea kwa duwa, asije katehemeka,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

Remmy Mwalo katibu mkuu, wa MUSSASi hadi sasa,
Mola mempa ruzuku, aongoza sawasawa,
Kamwe sitilii chuku, ye ni kiongozi mwema,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

Remmy mwenyewe mwungwana, mtu wa utaratibu,
Ni kijana kakawana, kwa wengi ye ni sahibu,
Haki 'tu atapigana, tukimpa ukatibu,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

Chuoni ameshaliki, maarufu kote kote,
Magharibi mashariki, kunaimbwa sifa zake,
Kusini na kaskazi, wamwambia chonde chonde,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

Tamati hino natuwa, kwa sharifu nawaacha,
Mwalo Remmy mwamjuwa, ila ninawakumbusha,
Mwalo Remmy amekuwa, mpe howe Chekwa Chekwa,
Mwalo Remmy ni mwenzetu, akuomba kura yako.

No comments:

Post a Comment