Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Sunday, 3 July 2016

COWESA UNGANA COWESA

Mboni nawakodolea, haya yangu pulikeni, 
Kidole nawanyoshea, naashiria wandani, 
Tafadhali si umbeya, COWESA myapateni, 
Ungana COWESA ungana, Umoja kitu muhimu. 

Majimbo yote ni sawa, nabaini kwa uchungu, 
Yanofanyika si sawa, na yanitia matungu, 
Wala msimee mbawa, kipungu hafikii mbingu, 
Ungana COWESA ungana, Umoja kitu muhimu. 

Ungana kaka ungana, dada yangu sikizeni, 
Tusije tukapingana, tukawa wawi mwishoni, 
Na tena tukabanana, tukashindwa namba wani, 
Ungana COWESA ungana, umoja kitu muhimu. 

Usimtweze mwenzako, maneno mengi tufyate, 
Kelele hina mashiko, tema mbali huo ute, 
Ama tuweke tambiko, au tukipige kite, 
Ungana COWESA ungana, umoja kitu muhimu. 

Ninalikunja suhufa, ninaimaliza sala, 
Tusichangie maafa, kwa kuifanya mikwala, 
Pamoja tuzibe ufa, na kuhepa madhila, 
Ungana COWESA ungana, Umoja kitu muhimu. 

#maleti mgonga chuma (mtunzi) 

No comments:

Post a Comment