Kwa kupigana huko, akajihakiki na kuona kuwa, ana uwezo wa kuaminiwa zaidi na kudai ukatibu mkuu wa chama hicho. Hapo ndipo kaa alipoanza kuinua gando. Ababu! Katibu mkuu! ODM! Hapana. Yaliyofuata ni MEN IN BLACK. Akapewa uongozi kwa kuhofia kuwa angesepa mapema. Akaukumbatia. Akarejelea mchezo wake kumtetea BABA yake/yao. Akawa tena kiongozi wa PAC. Kaa akainua gando tena. Akaitwa MOLE. Kisa! Anaegemea upande wa serikali saaaana. Baadaye akaondolewa kwa kudaiwa kuwa hafanyi makadirio ya matumizi pesa kwa njia bora. Kwa kuwa ni mtu aliyewatakia waliompigia kura mema, akaanza kufanya kazi na serikali. Ziara baada ziara katika ikulu kwa yale aliosema, kuzungumzia suluhu ya matatizo yanayomkumba mwanamlembe. Aliwaalika na kuhudhuria mikutano ya Rais na Naibu wake katika eneo la magharibi. Akaunda vuguvugu la wabunge wa magharibi waliloliita WESTERN COCCUS.Vuguvugu lililonuia kuwaleta wanamagharibi pamoja. Ziara ya Rais kule Mumias sugar company, alikuwapo. Mikakati ya kukifufua kiwanda cha Pan paper, alikuwa mhusika mkuu. Mikakati ya kuboresha kiwanda cha Kabras Sugar Company, alihusika. Vyote hivyo vikamweka katika kundi la fuko. Akaonwa kama msaliti. Wakasema AMEKULA VYA RUTO. Dhibitisho ya hayo? Jumba la kifahari na Ziara za nje ya nchi na mkewe.
Ngoma ikalia sana na hatimaye ikapasuka kiwambo. Huyo, akabeba vyake na kujiendea. Sababu za kuondoka zinajulikana na wengi, moja wapo ikiwa labda ya ;ivumayo haidumu. Amevuma saaana kule. LABDA. Mwenyekiti wa chama cha ODM kule Bungoma ambaye pia ni Mbunge wa Sirisia, meja John waluke, pia amepunga buriani chama hicho. Inasemekana kuwa, hata seneta wa Busia Amos Wako, anapanga vyake kwenye kasha lake, tayari kuwafuata wenzake. Labda, kati ya chama na wao, mmoja au wote ni simba wala watu, wakiliwa huwani?
Kando na ODM, uamuzi wake umempa nguvu kiongozi wa wachache katika seneti bwana Moses Wetangula ambaye amemwambia Raila kuwa, itafaa kabisa iwapo atamwunga yeye mkono katika uchaguzi ujao. Wetangula alisema katika mkutano wa hadhar katika kaunti ya Busia kuwa, eneo lake la magharibi lina wapiga kura wengi kuliko kinara yeyote katika CORD hivyo hakuna mjadala kuhusu atakayepeperusha bendera ya Urais. Kuna mnong'ono kuwa, Musalia Mudavadi na Weta watafanya mazungumzo ili mmoja wao awanie urais mwakani. Athari kuu ya Kisu cha ABABU NAMWAMBA.
No comments:
Post a Comment