Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Wednesday, 21 December 2016

HADITHI : MWIZI WA PENZI LAKE


Bwana Siwa alikuwa na rafikiye wa dhati waliopendana kwa hali na mali. Walikuwa wanatembeleana ; leo kwa Bwana Siwa kesho kwa yule rafiki. Mtindo huu wa kutembeleana ulifanyika kwa muda mrefu hadi yakawa mazoea. Marafiki hawa walikuwa wameoa na hivyo kutembeleana huko na urafiki baina ya waume hao ukafanya bibi hawa nao pia kuwa marafiki wakubwa. Nao pia, wakati mwingine walitembeleana manyumbani kwao. Vile vile, walivuka mipaka na hata kuanza kwenda mikutano ya chama pamoja na hata kanisani. Wakawa marafiki pia wa mate na ulimi.

Kumbe katika kutembeleana huko, Bwana Siwa alianza kumtamani mke wa rafikiye. Ndani ya moyo wake, tamaa ilikua na kuhanikiza kote. Ama kweli wanadamu siyo wema. Akaanza kumtongoza mke wa rafikiye kwa maneno matamu ila mke alikaa tisti. Siku moja akamsimisha na kumwomba, "wewe una mume na mimi nina mke, mbona tusiibe kidogo na iwe siri kati yetu tu, wasijue wao. ' mwanzo aliteta lakini baadaye akahiari. Siku iliyofuatia, mke huyo alimpigia simu Bwana Siwa asubuhi  ili amzuru kwake nyumbani. Siwa akafanya hivyo. Mwanamke huyo alikuwa amejipaka mafuta fulani yaliyonukia hadi Siwa akapenda. Walitoa ratiba ya jinsi mambo yatakavyofanyika usiku huo kwani mume wa mwanamke mwenyewe , ambaye ni rafikiye Siwa alikuwa kasafiri mbali. Mwanamke huyo akamwonyesha chumba watakachotumia pamoja na kitanda na kumwambia Siwa kuwa itimiapo saa tatu za usiku huo aje, afungue mlango utakao kuwa wazi na ampate kasarani tayari kumkabili. Walipokuwa wanaagana, mwanamke huyu akampapasa Siwa shavuni na shingoni huku akimsifu kwa misuli yake ambayo anatarajia imhudumie usiku huo. Wakaagana. Siwa alielekea kazini huku mwanamke huyo akisafiri hadi nyumbani kwa Siwa. Akampata mkewe Siwa akifanya kazi za nyumbani. Akaanza kumpa umbea. " shoga yangu tunapendana sana na sitaki kukuibia. Leo usiku nataka nikuonyeshe kile ambacho mumeo hutaka kunifanyia siku hizi zote."  akampa yale mafuta ambayo alikuwa amejipaka asubuhi hiyo alipokuwa na Siwa na kumwambia. " jipake haya mafuta na itimiapo saa mbili kasorobo uwe kwangu na nitakuelekeza jinsi ya kumkamata paka mnywa maziwa ya kuiba." akaahidi kufanya hivyo.

Saa tatu kasorobo mkewe Siwa alikuwa amekilalia kitanda cha rafikiye akingoja kumkata paka mnywa maziwa ya kuiba. Alinyamaza ji kama alivyombiwa na mwenyeji wake na kulala chali huku akiwa uchi samaki kando. Siwa akaja kwa hamu ya kuuwa mtu. Alitoa mavazi kwa haraka na kumsakama aliyekuwa kitandani kwa pupa. Alipoyanusia yale mafuta, akaamini kuwa ni mke wa rafikiye. Wacha kazi ifanywe kwa bidii na ustadi. Mitindo si mitindo. Alihema na kutoa sauti kama ya bata dume aliyemaliza mrimo. Mara, "oooh, beb wewe hukuumbwa ulitengenezwa. Wewe ni mtambo wa kutengeneza utamu kuliko nyuki, hakuna mwanamke kama wewe beb. Usiniache, ganda nami ili tunda hili tulile bila kuiba kama leo."  maneno hayo , Siwa aliyasema akiwa shambani, analima kweli. Mwanamke chini yake katulia, hatoi sauti ya kufanya ashuku lolote. Ingawa naye, kweli aliona Siwa kafanya kazi ambayo hajamfanyia yeye mkewe nyumbani. Baada ya kazi kuisha, mkewe ambaye alidhani kuwa ni mke wa rafikiye akapanua kinywa wakiwa bado kitandani na kusema, " mbona mume wangu hujawahi nifanyia yale ambayo umefanya leo tena kwa bidii hivi.?"  Siwa alishtuka na kuruka kutoka kitandani. Akawasha mwangaza mle chumbani na kuona kuwa kweli aliiba kilicho chake mwenyewe. Kumbe harufu ya mafuta ilimhadaa na kumfanya zuzu.

# merry christmas.. @kaka siwa(Twitter) . 

2 comments:

  1. Hello Mr Simiyu Hope this finds you well, I saw somewhere you have a manuscript almost through with and you are looking for the publisher. If you have not been successful to get a publisher Join the Gateway Publishers family today and make your dream a reality! We are always looking for authors and institutes who are interesting to publish their books; we ensure that your work reaches to more researchers, readers; we have the luxury of devoting more time and effort into publishing. We have a unique approach to publishing and provide authors with the highest quality books and the most inclusive benefits package available. Join the Gateway Publishers family today and make your dream a reality! Publish your book with Gateway Publishers Ltd.

    ReplyDelete
  2. Kindly contact me on +254- 0733379216/0721939428 email mecheoben@gmail.com .We have a unique approach to publishing and provide authors with the highest quality books and the most inclusive benefits package available. We are new upcoming publisher in Kenya

    ReplyDelete