Siku moja kijiji cha Nasaka kilijawa na habari za kuisha kwa dunia siku kadhaa zijazo. Watu walijaa fazaa na mahangaiko. Kunao waliochimba mashimo makubwa na marefu ili wajifiche humo wakati dunia itakuwa inateketea na kuisha. Wengine waliwaua wana na wake zao mapema eti wasiwaone wakiangamia dunia iishapo ilhali wengine walijitia vitanzi kwa woga na hofu.
Katika siku hizo, Bwana Siwa alikuwa pasta, muumini mcha mungu kupindukia. Alikuwa akihubiri katika kanisa lake, wapita njia barabarani walisitisha safari zao kwa minajili ya kusikiliza mahusia ya mtu wa mungu; Pasta Siwa. Wengi walimwogopa na kumpa heshima kuwa yeye ni nabii wa Mungu aliyesalia baada ya akina Eliya, Elisha na wengine kuondoka siku zile.
Pasta Siwa alipofikiwa na habari za kuisha kwa dunia siku kadhaa zijazo, jioni hiyo baada ya chajio, aliileta jamii yake ambayo ni mkewe, mwanawe Manga na Rukia na kuwaapiza. Kwa kuwa dunia ilikuwa inafikia mwisho wake, alitaka wote wakiri na kuungama dhambi zao hadharani ili yeye akiwa pasta awaombee radhi kwa mwenyezi mungu ili wasamehewe na kuridhi ufalme wa mbinguni baadaye . Rukia akaanza, " mimi baba na mama, wakati mama anaepukia nyama au mboga zozote kutoka mekoni, huzidokoa. Wakati mwingine hata mimi huziiba zikiwa zimewekwa kabatini. Hivyo ninakiri na kuomba msamaha" . Akamaliza. Manga naye akapanua mdomo, " mimi baba na mama, zile sarafu zote ambazo nyie huziweka kwenye kabati juu, mimi huzichukua na kwenda sokoni kuzichezea kamari na Lotto. Pia wakati mwingine mkinituma sokoni, chenji sirejeshi kamili hivyo ninakiri na kutubu." Akamaliza.
Pasta Siwa akamtazama mkewe na kuvuta hewa. Akaanza. " mimi mke wangu na wanangu wapendwa....mjuavyo ni mchungaji. Lakini nataka kukiri makosa yangu ila mwanzo ninataka wewe mke wangu uniahidi kuwa utanisamehe." Pasta Siwa akapeana masharti. Mkewe akaahidi kumsamehe. " asante." akaendelea. " basi mke wangu, takribani robo tatu ya wanawake katika kanisa letu, nime...nimeshiriki nao mapenzi zaidi ya mara moja. Yaani nimezini nao mara kadhaa na hivyo ninakiri mke wangu na wanangu na kutubu." Akamaliza.
Mkewe naye ikafika zamu yake. Akamtazama pasta Siwa pia na kuvuta hewa. " mume wangu, hili ni lako. Nami pia kabla sijalisema, naomba uniahidi kuwa utanisamehe na hutanifukuza humu mwako." Pasta Siwa akahiari kumsamehe kwa lolote. "hivyo basi nisikilize pasta, tena tia makini. Kwa hawa watoto wawili; yaani Manga na Rukia, hakuna damu yako. Kwa maana si wako licha ya wewe kuwalea na kuwaona kama wanao." Pasta Siwa alianguka kutoka kitini pu kama gunia la mahindi. Hadi hadithi hii ikitamatika,pasta Siwa hajaamka.

No comments:
Post a Comment