Usiku mmoja ; usiku wa kiza cha kutisha usiokuwa ma mbalamwezi katika kijiji cha Nasaka, watu wawili walikutana katika boma la tajiri fulani bila kutarajiana. Mmoja alikuwa mchawi wa kukimbia usiku ambaye alifanya hivyo kila usiku roho za mababu zake zikimwamka. Alikimbia ili kujipoza angalau. Wa pili naye alikuwa mwizi. Huyu hakudhamiria kuiba kimabavu. Huyu ni wale waitwao wezi wa njaa, hataki pesa wala vitu vya dhamana bali kwake chakula ndicho cha muhimu. Ikiwa ni huku kwetu, basi wezi aina hii wangeangamiza gala lako la mahindi posho lako la unga bila kusahau sukumawiki na mkunde kitaluni.
Walikutana uwanjani katika boma la bwenyenye, kila mtu akiwa kwa shughuli yake. Watu hawa waligongana kutokana na kutokuona kizani. Loh! Kila mtu mguu niponye akidhani kuwa labda amekutana na mwenyeji wa boma hilo au mlinzi. Walikimbia kila mmoja na kwa nasibu wakatumbukia kwenye shimo moja refu ambalo tajiri huyo alichimba karibu na ukingo wa uwa wake.
Mle shimoni, aliyekuja kuiba akatoa kikurunzi kidogo alichokuwa amekibanza kwenye nguo na kukiwasha. Kila mmoja alitazama mwenzake na kugundua kuwa ni watu wawili tofauti ambao hawajuani. Wakaulizana kuhusu shughuli zilizowaleta humo bomani na mchawi akasingizia roho za mababuze huku naye mwizi akisingizia njaa. Wakasaidiana na kutoka humo shimoni
Tangu hapo, mwizi yule wa njaa na mchawi wa kukimbia usiku walishirikiana kwa kuwahangaisha wenyeji wa kijiji cha Nasaka. Wakaaji wa kijiji hicho mpaka leo wanaishi kwa hofu kutokana na genge hilo la watu wawili. Piga darubini katika nchi yako na viongozi waliomo kisha ung'amue maana ya hadithi hii ya kimafumbo.

No comments:
Post a Comment