Kila masika hayakosi mbu. Naam, hasa nchini Kenya. Uchaguzi ukaribiapo, mbu wa ukabila huja na kumwuma kila yeyote aliyedhania kuwa kasimama tisti na uzalendo. Mbu hawa wa ukabila husababisha magonjwa kama vile chuki miongoni mwa marafiki, uchochezi kwa wale wajuao haki ya kujieleza na hata ubishi na mapigano kwa wale wenye nguvu kuliko goliathi na samsoni.
Msimu huu nao, mbu hawa wameleta gonjwa jingine tofauti. Kurarua nchi ili nasaba ya kuongoza iwe na nchi yao tofauti na nasaba ya kuongozwa. Swala hili limezua mhemko wa aina yake kwa wale 'tulio katika upinzani' na wasiwasi mkubwa kwa wale werevu wachache nchini. Kurarua nchi ili kuiacha nasaba ya uongozi iwe na nchi yao ni swala zurii kwani litawapa wale wenye tamaa ya kukikalia kigoda cha uongozi nafasi ya kufanya hivyo kabla ya kustaafu au kuuka, ashakum si matusi. Tena litatenga jamii 'zinazojiona' kuwa safi kando na zile zinazodaiwa kuwa ni za wizi, ufisadi na unyakuzi wa mashamba miongoni mwa mabaya yote yaliyowahi kuwa duniani. Naam, swala hili la kuirarua nchi litapunguza unyakuzi wa mashamba, litaleta usawa na labda kila mwanachi wa nchi hizo za udhanaishi atajivunia nchi yake. Labda kiwango cha uzalendo ambacho kimeshuka miongoni mwa wanachi, kitapanda hadi zaidi ya asilimia 100. Ama kweli, Kurarua nchi kutaleta manufaa mengi chambilecho wararuzi.
Kurarua nchi kwa kiasi fulani kunachangiwa na jazba ya kuongoza kwa wale ambao bado hawajapata nafasi hiyo. Lakini swala kuu si hilo. Ukabila. Chuki ya kikabila ndio mhimili mkuu wa kurarau nchi. Makabila ya watawaliwa pia nayo yanataka yapewe nafasi. Makabila haya yamkinika hayajaonja matunda ya demokrasia achilia mbali huru. Yanahisi kuwa mara kwa mara ushindi wao hunyakuliwa na mwewe waoteao juu ya miti mikuu na ambao hunyakuwa vifaranga wa demokrasia yao na kuwapelekea makabila ya watawala. Ni bayana kuwa madai haya ni kweli na ni juzi tu, tangu mzee Jomo na Jaramogi kupiga dunia teke, tumeona angalau makabila ya watawaliwa yakionja utamu wa kushinda kwa kurejeshewa mayai ya demokrasia yao ili wayaatamie tena na kuyaangua oktoba 17 ilhali makabila ya watawala kwa mara ya kwanza yameonja uchungu wa ushindwe. Kwa mtawaliwa ikawa asali na kwa mtawala ikawa shubiri. Lakini kwa yeyote mwenye jicho pevu, ni aidha asali chungu au shubiri tamu ; inategemea jina lako la pili na kule anakovutia kamba 'mkubwa wako'.
Sidhani kuwa nitakosea nikisema kuwa, nchi hizi za udhanaishi zitakuwa na makabila ikiwa nchi kuu itararuliwa. Nchi dhanaishi ya watawaliwa itakuwa na makabila mengi kuliko nchi dhanaishi ya watawala. Jambo ambalo kila mmoja ataniunga mkono ni kuwa katika kurarua nchi, wananchi wa nchi zile dhanaishi ni wale wale. Ni sawa na kundi la ndege lilohama mti mkuu fulani na kujenga viota katika mti mwingine lakini ni wale wale, wenye manyoya yale yale na wenye milio ile ile. Kuna Uwezekano mkubwa kuwa, sababu ndege wametengeneza nchi mpya ila tabia ni zile zile, basi kilichowafanya kurarua nchi pia wamekibeba, hawajakiacha nyuma. Utafikia wakati ambapo kabila moja pia katika nchi hizo dhanaishi litaonyesha ukiritimba mkubwa katika kukikalia kigoda na kugawa nyama. Yale makabila mengine pia yataanza kulalamika na matokeo yake, kama awali, nchi ile mpya dhanaishi itararuliwa na nchi nyingine kubuniwa. Na kwa kuwa bado ndege wana tabia zile zile, huenda nchi zile pia zikararuliwa na kutengeneza nchi nyingine. Mwisho wa siku, Kenya iliyokuwa nchi moja na yenye kaunti 47, huenda likawa sasa bara lenye nchi 47 ; kila nchi ikiwa ya watu wa kabila fulani tu. Itakuwa heri labda kwa nchi iliyobuniwa na watawala wa bara la Kenya awali kwani, makabila haya mawili huenda yakasilizana kuongoza kwa zamu, leo hawa kesho wale. Kazi kikoa. Tabu kubwa itakuwa ni kwa wenzao.
Enga 'wararuzi'. Kogeni uso ndipo mtoke nje. Nchi itabadilika tu ikiwa chandarua cha ukabila kilichozunguka akili zetu na ambacho hufukuza urazini wetu wakati wa uchaguzi, tutakitoa ili turuhusu sera kuwa kigezo cha kuchagua bali si jina la pili la mgombea. Rarua chandarua hicho cha ukabila kabla ya kufikiria kurarua nchi yetu.

No comments:
Post a Comment