Rasimu ya katiba mpya ya MUSO imegawanywa katika Sura kumi na takribani ibara sitini na tano kulingana na tolea la tatu la rasimu ya katiba hiyo ya mwaka wa 2016.
Sura ya pili ya rasimu hii inahusu uanachama, uongozi na maadili pamoja na hazina ya MUSO. Sura ya tatu inazungumzia muundo au mpangilio wa uongozi katika chama chenyewe. Hapa, utapata viongozi pamoja na majukumu wanayofaa kutekeleza, kando na ratiba ya mikutano ya chama. Sura ya nne ya Rasimu hii inazungumzia bunge la Congress. Katika ibara ya ya 17, kunazo njia za wazi za kuteua wanachama wa bunge hili nayo ibara ya 20 inatoa bayana majukumu ya wanachama wa bunge hilo la Congress.
Ibara ya 31 inaeleza kuhusu kamati za bunge hilo ambazo ni :
Kamati ya fedha na uwekezaji
Kamati ya usalama, malazi, afya na ustawi wa wanafunzi.
Kamati ya michezo na burudani
Kamati ya elimu, maktaba, habari, machapisho na uhusiano wa nje.
Sura ya tano inaangazia Fedha na Uwekezaji. Ibara ya 33 na 34 inaeleza jinsi MUSO itakapopata fedha zake na namna ya kusanya ushuru. Ibara 35 inazungumzia jinsi MUSO itakavyotumia fedha hizo. Ibara za 36,37,38,39 na 40 zinaelezea hazina ya MUSO, wasimamizi wa hazina hiyo na mbinu za uwekezaji wa chama. Sura ya sita inaangazia Uchaguzi mkuu na uchaguzi mdogo. Ibara ya 43 katika sura hiyo inazungumzia sheria za uchaguzi ,45 inaelezea makosa ya uchaguzi, 46 inaangazia uchaguzi mdogo wa wabunge wa Congress, 47 inazungumzia duru ya pili ya uchaguzi huku ibara za 49-52 zikizungumzia kesi za uchaguzi, uchaguzi mdogo na kuapishwa kwa viongozi.
Kwa kiduchu tuangazie SURA YA TATU ; Muundo wa Uongozi wa MUSO.
Vyombo au Viungo vikuu vya MUSO kulingana na ibara ya 8 ni :
Baraza la uongozi wa wanafunzi
Bunge la Congress
Mkutano wa jumla wa kila mwaka ( A. G. M)
Mkutano spesheli wa jumla (S. G. M)
Na viungo vingine vitakavyoidhinishwa na baraza la uongozi.
Ibara hiyo hiyo ya nane pia inabainisha wanachama wa baraza la Uongozi wa wanafunzi ambao ni :
Mwenyekiti
Naibu wa mwenyekiti
Katibu mkuu
Katibu wa fedha
Katibu wa Elimu
Katibu wa maswala yasiyo ya kiakademia.
Katibu wa mahitaji spesheli na maswala ya kijamii.
Katika uchambuzi ujao, tutaangazia Majukumu ya Baraza la uongozi wa wanafunzi, kuondoka ofisini kwa mwanabaraza na pia muda wa kuhudumu wa mwanabaraza la uongozi wa wanafunzi.
Toa maoni yako kwenye blogi hii pale chini kisha unifuate (follow my blog) ili kuelimishana zaidi. IJUE KATIBA YA MUSO.

No comments:
Post a Comment