Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Monday, 2 April 2018

MUUZA DAWA


Ewe muuza dawa,
Usijione daktari,
Sindano ukanidungua,
Usijifanye kuwa nesi,
Maswali kuniuliza,
Nijapo dukani,
Zichukue zangu pesa,
Usinisumbue!

Ewe muuza dawa,
Hilazo metambua,
Udaktari wajitia,
Hela zangu kuzivua,
Mnununzi nikifika,
Usijaribu kunidodosa,
Pesa zangu chukua,
Usinisumbue!

Ewe muuza dawa,
Ni biashara unafanya,
Zamani nemkujua,
Udokta hukusomea,
Tafadhali kikueleza,
Nipokeze hizo dawa,
Sijaribu kunidondoa,
Kiundani kunijua,
Usinisumbue!

Ewe muuza dawa,
Mfanowo shopukipa,
Hela kuzitafuta,
Kiburi situmia,
Sijaribu lazimisha,
Hela nyingi kupokea,
Hadharani nakwambia,
Uwache kunidodosa,
Usinisumbue!

Ewe muuza dawa,
Nikupe kumbukumbu,
Jana likujia,
Kununua kondomu,
Nakwambia ulinisinya,
Kwa hizo zako chuku,
Mimi ninavyojua,
Kondomu ni kondomu,
Siku nyingine nikija,
Usijifanye kunikimu,
Usinisumbue!

Ewe muuza dawa,
Mchumba limtuma,
Aje kwako duka,
Pili Kununua,
Maswali mbona sasa,
Kaziye kujua,
Usjifanye kuwa duma,
Kutafuta lichoficha,
Uza dawa,
Usinisumbue!

2 comments:

  1. Haha hongera kwa kazi nzuri.Kwa kweli kununua iyo Kondoo kama Mwaibale alivyoiita ni ngumu.Muuza dawa anachunguza waenda kutumia na nani.

    ReplyDelete