Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Friday, 6 April 2018

NAKARIBIA NDOA!

       
Nakaribia ndoa,
Ishirini na tano megonga,
Tangia lipozawa,
Mengi mepitia,
Mabonde na milima,
Hapa lipofika,
Nashukuru maulana,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza.
          Nisubirini!
 
          Nakaribia ndoa,
Kijichuna najiona,
Ngozi mekomaa,
Msuli meujaza,
Maisha kuelewa,
Ufahamu mepata,
Jinsi kuwajibika,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
          Nisubirini!

         Nakaribia ndoa,
Masomo nakamilisha,
Sokoni tajimwaya,
Darubini nitapiga,
Kazi kitafuta,
Kikosa kuajiriwa,
Kujiajiri taamulia,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
        Nisubirini!

        Nakaribia ndoa,
Nyanyangu kanieleza,
Nisije nikachelewa,
Ufupi wa maisha,
Kizembea tadhurika,
Ishirini na tano megonga,
Kaburi lapanuka,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
         Nisubirini!

         Nakaribia ndoa,
Mwana lipozawa,
Mamangu na baba,
Mengi watarajia,
Jamii kuendeleza,
Naahidi kutozembea,
Wasaa ukifika,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
        Nisubirini!

         Nakaribia ndoa,
Hirimu yangu nawambia,
Usingizini zindukana,
Maji yamekupwa,
Samaki tuwavua,
Msije damu laza,
Upepo mtageuka,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
         Nisubirini!

        Nakaribia ndoa,
Maoni nakaribisha,
Na maelekezo ya wakubwa,
Ushauri sikataa,
Ya wenge wanonipenda,
Nisaidieni kusukuma,
Mtubwi wangu kuelea,
Mwakani inshallah,
Taarifa taitangaza,
          Nisubirini!

4 comments: