Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Tuesday, 10 April 2018

Tafsiri ya Shairi (ENDIKA - BAISKELI)

BAISKELI
Baiskeli ya kwangu,
Yasikize yalo yangu,
Nilikuleta kwangu,
Sababu ya penzi langu,
Kipenda uwe wangu,
Usiwe ja kindoo,
Watu wakuzungushe-zungushe.

Ghala langu sasa,
Sijivune kwa sura,
Ukadhani ni chakula,
Kaogopa na masizi,
Kakataa kwenda mekoni,
Ati ni kuharibu sura,
Linunua sufuria hiyo,
Kakupa ikawa yako,
Siniue kwa njaa,
Ati wahifadhi sura.

Nilikuwa mbali mashambani,
Kamulika macho nyumbani,
Kamwona kapera na rungu,
Kabeba sukari mkononi,
Akaja na matamu maneni,
Ndo umpe kilicho mafichoni,
Baiskeli nakutegemea kweli,
Usinilinge jiwe kisogoni.

Hata uwe mweupe pe!
Au uwe mweusi ti!
Sijivune na kuringa la.
Dunia takuning'iniza juu,
Ulie machozi kupukupu
Dunia hii si tamu,
Sifikirie tu utamu,
Mhenga alishanena,
Mali ni makuyu

No comments:

Post a Comment