VAR HUJUMAAAAA!!
Afrika muondokeni, mrudini bara letu,
Muondoke uzunguni, mkajenge bara lenu,
Mmeyaona hadharani, yalowapata waldikapu,
VAR mnyama gani, asiyeona ya weusi,
VAR ni hatari, ni mnyama aseadabu,
Anaiba hadharani, haogopi na mtutu,
Anyakua mdomoni, hata kiwa ni kwa nguvu,
VAR mnyama gani, asiyeona ya weusi!
VAR kitimbakwiri, ubinafsi ameudumu,
Meibia senegali, kahakikisha sifaulu,
Meondolewa shindaoni, kawapandisha na matatu,
VAR mnyama gani, asiyeona ya weusi?
VAR bovu nazi, lahanikiza mbaya harufu,
Halitupendi asilani, metujazia machungu,
Ufungwa metutiani, uhuru wetu meusahau,
VAR mnyama gani, asiyeona ya weusi.
memwagika hayazoleki, waldikapu imetupiku,
Tumeondoka uzunguni, mewaachia yao mizungu,
Turudini nyumbani, tukuze bara letu,

No comments:
Post a Comment