Tunga, tunga shairi,
Shairi la kijiti,
Kijiti kidigi,
Kidigi shinani,
Shinani pana mizizi,
Mizizi ilokita.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kimti,
Kimti cha matawi,
Matawi na majani,
Majani ya kijani,
Kijani iliyokoza
Tunga, tunga shairi,
Shairi la mti,
Mti wa mchikichi,
Mchikichi msituni,
Msituni gizani,
Gizani kusiko mwanga
Tunga, tunga shairi,
Shairi la vijabali,
Vijabali viwili,
Viwili shinani,
Shinani pa mti,
Mti ulokomaa
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kisiki,
Kisiki cha mti,
Mti uso matawi,
Matawi yaso majani,
Majani yalikauka.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kidibwi,
Kidimbwi mjini,
Mjini kimejisetiri,
Kimejisetiri vizuri,
Vizuri kinapendeza.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la safari,
Safari ya maji,
Maji ya kisiki,
Kisiki Kidimbwini,
Kidimbwi kikaloa.
Shairi la kijiti,
Kijiti kidigi,
Kidigi shinani,
Shinani pana mizizi,
Mizizi ilokita.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kimti,
Kimti cha matawi,
Matawi na majani,
Majani ya kijani,
Kijani iliyokoza
Tunga, tunga shairi,
Shairi la mti,
Mti wa mchikichi,
Mchikichi msituni,
Msituni gizani,
Gizani kusiko mwanga
Tunga, tunga shairi,
Shairi la vijabali,
Vijabali viwili,
Viwili shinani,
Shinani pa mti,
Mti ulokomaa
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kisiki,
Kisiki cha mti,
Mti uso matawi,
Matawi yaso majani,
Majani yalikauka.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la kidibwi,
Kidimbwi mjini,
Mjini kimejisetiri,
Kimejisetiri vizuri,
Vizuri kinapendeza.
Tunga, tunga shairi,
Shairi la safari,
Safari ya maji,
Maji ya kisiki,
Kisiki Kidimbwini,
Kidimbwi kikaloa.

No comments:
Post a Comment