Bahari ilo shwari, hi'toa mwanamaji stadi,
Mmeyapitia yalo mengi, lipokuwa safarini,
Majeraha ya wachezaji, yaliwapa wasiwasi,
Heko harambee stars, mmechuna miamba,
Mlimkosa wanyama, Mariga na Masika,
Vifyefye wakamuona, dharau ikahanikiza,
Fimbo mmewachapa, chooni watalilia,
Heko Harambee Stars, mmetupa furaha ,
Mmefua tumaini, la kufuzu mwakani,
Mmerejea meelini, hadi ng'ambo kusafiri,
Heri twawatakieni, kwa yote ya mbeleni,
Heko Harambee stars, meondoa jinamizini,
Mashabiki walojima, uwanjani kujituma,
Sauti zao lihanikiza, ili moyo kuwapatia,
Sitakuwa mkiritimba, pongezi kuwanyima,
Heko Harambee Stars, mmepaa nguuni.
Nawarai wasimamizi, wizara na serikali,
Mjitume kila hali, kushajiisha wachezaji,
Mzitenge fulusi, kufadhili na kuzawidi,
Heko Harambee stars, ushindi umetufaa.
Tamati ninapotua, wakenya na Afrika,
Muondokeni ulaya, mrejee kwenye bara,
Vilabu vyetu shangilia, mchezo kuukuza,
Heko Harambee Stars, macho metufungua.
@Tungo za Daniel kaka Si'wa
Nasaka - Bungoma
0725727519
Mmeyapitia yalo mengi, lipokuwa safarini,
Majeraha ya wachezaji, yaliwapa wasiwasi,
Heko harambee stars, mmechuna miamba,
Mlimkosa wanyama, Mariga na Masika,
Vifyefye wakamuona, dharau ikahanikiza,
Fimbo mmewachapa, chooni watalilia,
Heko Harambee Stars, mmetupa furaha ,
Mmefua tumaini, la kufuzu mwakani,
Mmerejea meelini, hadi ng'ambo kusafiri,
Heri twawatakieni, kwa yote ya mbeleni,
Heko Harambee stars, meondoa jinamizini,
Mashabiki walojima, uwanjani kujituma,
Sauti zao lihanikiza, ili moyo kuwapatia,
Sitakuwa mkiritimba, pongezi kuwanyima,
Heko Harambee Stars, mmepaa nguuni.
Nawarai wasimamizi, wizara na serikali,
Mjitume kila hali, kushajiisha wachezaji,
Mzitenge fulusi, kufadhili na kuzawidi,
Heko Harambee stars, ushindi umetufaa.
Tamati ninapotua, wakenya na Afrika,
Muondokeni ulaya, mrejee kwenye bara,
Vilabu vyetu shangilia, mchezo kuukuza,
Heko Harambee Stars, macho metufungua.
@Tungo za Daniel kaka Si'wa
Nasaka - Bungoma
0725727519
Kongole Mwalimu
ReplyDeleteAsanAsa
Delete