Katika kijiji cha Nasaka ndiko alikoishi bwana Siwa na mkewe. Walikuwa wamejaliwa na mtoto pekee katika kipindi chote cha ndoa na mkewe. Mtoto mwenyewe walimwita Manga. Pamoja nao, alikuwa mamake Siwa Bi Namaemba ambaye alikuwa kakonga kweli.
Baada ya miaka miwili hivi Bi Namaemba aliaga dunia. Siwa na familia yake walifanya juhudi na kumzika mwendazake kwa njia ya heshima kweli. Watu waliohudhuria matanga walikula na kufurahi mpaka. Si ugali wa wimbi na ule wa mahindi, si wali, si pilau, si nyama-ng'ombe pamoja na nyama-kuku. Kwa walevi ilivyoada kijiji, kulikuwa na pombe ya kugemwa nyumbani ; chang'aa na busaa. Walishughulikiwa vyema kweli.
Mwezi mmoja baadaye, Bwana Siwa alihamia ng'ambo ya pili ya mto sichei, mahali kulikoitwa Luuya ambako alinunua shamba kitambo kidogo alipolipwa 'pesa za miwa'. Kule, maisha hayakuwa mazuri. Licha ya kuwa mkewe hatimaye alifanikiwa kushika mimba tofauti na awali, mkosi wa vifo vya watoto wachanga waliozaliwa vilizidi. Kila mtoto alipofikisha miezi miwili baada ya kuzaliwa, alifariki ghafla bila hata kuugua. Mchanga ulimeza watoto watano wa bwana Siwa ambao cha kushangaza hawakuugua. Kukatokea mzee Kasawa ambaye alikuja na kumwarifu kuwa, ili kusitisha vifo hivi, Bwana Siwa alitakiwa kwenda 'kumtengeneza' nyanyake kule Nasaka alikozikwa. Alitakiwa kufanya tambiko kama mila ilivyotaka kwa kumchinja mbuzi mweusi kwenye kaburi la Marehemu mamake na baada ya hapo, wanawe wachanga hawangefariki tena.
Basi asubuhi ya siku iliyofuatia, alimchukuwa mbuzi mweusi katika kundi la mifugo wake wengi na pamoja na mwanawe Manga, wakafunga safari ya kwenda Nasaka kufanya matambiko hayo. Walitembea kwa muda na kuufikia mto Sichei. Loh! Babamtu kashikwa na kitefutefu, hajielewi. Mwili si wake tena. Alitapatapa kama mtu aliyeugua malaria. Aliuweka mkonowe kwenye mfuko wake wa koti lake kuukuu na kupigwa na butwaa. Kumbe hakuwa amebeba 'dawa yake' ambayo ni sigara. Bwana huyu alikuwa mraibu wa sigara kupindukia. Akamwambia mwanawe akimbie hadi kwenye chumba chake cha kulala kule nyumbani na chini ya pilo ya kitanda chake, achukue sigara moja amletee pamoja na kiberiti. Siwa akaahidi kumngoja mwanawe.
Manga alikimbia na kufika nyumbani. Bahati, mlango wa nyumba ulikuwa umeshindikwa tu. Akaufungua bila kubisha na kufululiza hadi kwenye chumba cha kulala cha wazazi wake. MAAJAB! Alimfumania mamake na mzee Kasawa wakiramba asali haramu wasisikie hata akija. Yaonekana asali ilikuwa tamu sana kwani hawakuhisi uwepo wa mtu katika chumba hicho. Manga aliushindika mlango huo pole pole na kwa haraka akasema lazima hili limfikie babake Siwa. Alikimbia na kufika katika mto sichei. MAAJAB! Katika kichaka kando ya mto Sichei, alimfumania babake pia. Bwana Siwa alikuwa amejigeuza beberu au tuseme kamgeuza mbuzi kuwa mke. Angemshtaki nani na kwa nani? Ni nani kati ya wazazi wale mwenye kosa kubwa zaidi? MSURURU WA HADITHI ZA MANGA, MBILIKIMO MJANJA UTAENDELEA. lakini jibu maswali hayo kwenye 'comment box' tafadhali na ufuate blogi yangu hii pia tafadhali.
Facebook : kaka siwa
Twitter : @kaka siwa

Great brother
ReplyDeletethanks kaka...
Delete