Tarehe za uchaguzi zilitangazwa juzi. Ni jambo la kusikitisha sana kuona jinsi wagombea wa nyadhifa mbalimbali wanaendeleza kampeni zao za pembeni bila ufahamu wa katiba mpya ya MUSO. Je, wewe ukiwa mpiga kura, una uwezo wa kumchagua nani moja kwa moja? Na je, mgombea yeyote katika nyadhifa kuu atachaguliwa na nani? Katika toleo hili la pili la IJUE KATIBA YA MUSO, tutaangazia hatua za upigaji kura kutoka tarehe ya mwanzo hadi kuapishwa kwa viongozi.
Duru ya kwanza ya Uchaguzi itahusisha uchaguzi wa wajumbe ambao watasimamamia vitivo mbalimbali. Kulingana na katiba hii mpya, vipo takribani vitivo kumi na vimoja kutoka mabewa yote tisa ya chuo kikuu cha Moi.
Bewa kuu litakuwa na Vitivo vitatu vya uchaguzi ilhali mabewa shirikishi yatakawa na kitivo kimoja cha uchaguzi kote katika kila bewa.
Orodha ya vitivo ni kama ifuatavyo
:
Bewa Kuu (vitivo vitatu vya uchaguzi)
(kitivo 0001) : kitivo cha Elimu, Kitivo cha Uchumi na biashara, Kitivo cha Sayansi ya Mawasiliano.
(kitivo 002) : kitivo cha sanaa na Sayansi za kijamii, Kitivo cha Ustawi wa Raslimali za kibinadamu .
(kitivo 0003) : Kitivo cha Kilimo na sayansi za asili, Kitivo cha bayolojia na sayansi fizikia.
(kitivo 004) : Bewa la Annex
(kitivo 005) : Bewa la Mjini Eldoret.
(kitivo 006) : Chuo cha sayansi ya Afya.
(kitivo 007) : Bewa la Eldoret Magharibi.
(kitivo 008) : Bewa la Kitale
(kitivo 009) : Bewa la Kericho
(kitivo 010) : Bewa la Nairobi
(kitivo 011) : Bewa la Pwani.
Kulingana na Ibara ya 43 A (19) inayozungumzia utaratibu na sheria za Uchaguzi, Washindi watatu wa kwanza ndiyo watakao kuwa wajumbe wa kitivo chochote kile. Lakini vipo vikwazo vifuatavyo :
(1) Ikiwa washindi watatu wa kwanza watakuwa watu wa jinsia moja, basi aliyeibukia wa tatu atachujwa na nafasi yake kuchukuliwa na mshindi wa kwanza katika ile jinsia nyingine
(2) Ikiwa nambari tatu na nne watakuwa na kura sawa na tayari nambari moja na mbili ni watu wa jinsia tofauti, basi mwenyekiti wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi atakuwa huru kuitisha duru ya pili ya uchaguzi kati ya washindi waliopata kura sawa.
Wawakilishi wa Vitivo ambao watachaguliwa hapo ndiyo watakaokuwa wajumbe na pia wabunge wa Bunge la Congress. Kuchaguliwa kwa wajumbe hao kutakuwa mwisho wa Duru ya kwanza ya Uchaguzi.
Duru ya pili ya uchaguzi, ambayo imeratibiwa kufanyika tarehe saba Oktoba, itahusisha wajumbe ambao walichaguliwa kuwakilisha vitivo mbalimbali (kitivo 001 hadi kitivo 011). Katika Toleo la tatu, tutaangazia taratibu za kuchagua Viongozi wakuu wa MUSO.
Ikiwa ulikosa Toleo la kwanza, basi fuata wavuti huu :
#WWW.simiyukaka.blogspot.co.ke/2017/09/ijue-katiba-ya-muso.html?m=1
*kumbukeni kuwa juma lijalo kipo kipindi kipya zaidi katika redio ya MU FM 103.9. KIU ni kipindi kitakachozungumzia utamaduni wa makabila yote ya nchi Kenya na Kitajumuisha KAKA SIWA, DICKSON MATIABE NA MUKAH MATHEW. Jongea tujuzane kuhusu usuli wetu. usikose kutusikiliza...

No comments:
Post a Comment