Kunajisi ati ni pepo la tamaa waama. Labda. Maendeleo kiteknolojia, uzungu unaomiliki fikira zetu na uhuru ambao baadhi ya viumbe walilazimishiwa ndicho kichocheo hasa cha Pepo hili la kunajisi au kubakwa, ikiwa kweli ni pepo. Ukilinganisha maisha ya wazee wetu na maisha ya ujana wetu, utagundua kuwa ipo tofauti kubwa sana. Jambo la kimsingi si tu elimu na fikira bali hata maadili. Ni kweli kwamba elimu ya wazee wetu ilikuwa mbovu ikiwa si butu, lakini pia sikosei nikisema, katika ujana wao, walijiheshimu kutuliko. Walikubali sana Uafrika wao na walikuwa tayari kuutetea. Alisema rais wa zamani wa Marekani Theodore Roosevelt kuwa, Kumwelisha mtu kiakili na si kitabia ni kuelimisha hatari katika katika jamii. Ndiyo hali halisi ukizingatia jinsi wanawake wanatumia elimu yao ya sasa.
Tazama mkondo wa mavazi watoto wa kike wa sasa na wa zamani. Zamani naambiwa pia wazee wetu hawakuwa na nguo ila baada ya majilio ya mzungu mmishonari ambaye badaye alitukoloni na kuondoka na akili zetu, waliweza kupata nguo. Nafikiri mama zetu ni vielelezo tosha kuhusu jinsi walivyovaa wakiwa wasichana. Sketi ndefu na zinazositiri mwili, walificha vyote ambavyo 'ni haki tu kwa waume zao kuona pekee' na waliheshimu majira. Lakini wa sasa je? Minisketi, migongo wazi hata kama imejaa mabaka meusi kama mikono ya mhunzi, vitovu nje, maziwa yananinginia tu kama mbwa anayenyonyesha na mengine mengi ambayo yamezoeleka kwa mwanamke wa chuo kikuu ambaye anafahamu uhuru wake na aliye na elimu bam bam.
Saa za kuwa ndani ya nyumba ni kabla ya saa tatu kwa mtoto wa kike anayejijali. Lakini kunasikika kuwa hata saa nane, usiku mkuu mtoto wa kike yuatembea nje? Kwa vigezo hivi, anapofanyiwa madhila, tunalaumu pepo. Pepo alaumiweje ilhali umemwita wewe? Ni sawa na kulipa dudu liumalo dole lako, litakuuma. Ubakaji ni bayana kuwa haufai. Lakini mwanamke kuelekeza ulimi wake kwenye shimo la mchwa halafu akiumwa analilia usaidizi kwa kusema kuwa kaonewa, si ungwana.
Komredi kubeba mabango na kuvua mashati kwa kumtetea mwenzao aliyedai kabakwa ni jambo la kushangiliwa sana. Lakini nitafurahi ikiwa komredi yuyo huyo atamfunza mtoto wa kike jinsi ya kuvaa mavazi ya heshima na saa za kuwa chumbani mwake. Kumbukeni kuwa, kinga ni bora kuliko tiba. Tusibebe mabango baada ya mtoto wa kike kubakwa ila tumfundishe jinsi ya kuepuka kubakwa.
Kuno,
Kubakwa kutakuwapo,
Bora tu endapo,
mtazidi na yenu maguo,
Ya kuonyesaha yenu maungo,
Yanayochakaza za kubaka pepo.
Nduli na mchimba dawa,
Shauri lao moja.
Marehemu shaaban Robert kwenye Riwaya ya Utubora aliandika kuwa:
Adabu ni dhahabu,
Na johari ya moyo,
Na mstaarabu,
Ni mwenye kuwa nayo,
Na mbele ya aibu,
Kitu hiki ni ngao. (Shaaban Robert)
*kumbuka kutusikiliza jumanne hii katika MU fm 103.9 kuanzia saa kumi jioni hadi kumi na moja tukiangazia safari ya jamii za Kenya kutoka Congo hadi makazi yao ya sasa katika Kipindi cha KIU. Penda ukurasa wetu wa Facebook KIU.

No comments:
Post a Comment