Januari mosi,
Haupo hausikiki,
Haupo machi,
hadi juni,
Hausikiki julai,
hadi novemba mwishoni,
Mwanangu anisaili,
Utafika lini,
Krismasi?
Mwaka jana ulipokuwa,
tulifurahia ghaya,
Kuku walichinjwa,
sharubati tukanywa,
Chapati na shamrashara,
tukavaa mpya mpya,
Yote tuliyafanya,
ili wewe kukupamba,
Mwanangu anisaili,
Utarejea lini,
Krismasi?
Kutu kuu ya izraili,
Kwa hamu twakusubiri,
Ufike kwetu mastakimuni,
Tuvae vilivyofichika makashani,
Tule vilivyobanzwa makabatini,
Tulie vilivyofukiwa magodoroni,
Tulalapo kitandani,
Tulale si ka' zamani,
Ulipoadimika usingizi,
Na mguso wa mkeangu laini,
Mkeangu anisaili,
Utafika lini,
Krismasi?
Ama wewe mwizi mkuu,
Uliniibia wangu kuku,
Ukaiba bashasha zangu,
Kwa ugomvi na mkeangu,
Alitaka vazi kuntu,
avae katika mashamshamu,
Aliniumiza sana wengu,
Aliponenena, 'acha nende zangu,'
Kwa takwale kulikufuru,
Akinisaili mwanangu,
Nitamhaada kuwa huku,
Hutatia lako guu,
Krismasi!
Ingawa kanihadaa sineni,
karo ya shule sinani,
zafungua mwakani,
Wanangu wa' mgongoni,
Wanidai "baba, nitatiani begini"
Pesa sina sinani,
Sauti yanicheka akilini,
" mpumbavu kalaghaiwa hadharani,
Ulidhani ya siri hatutayabaini! "
Mwangu akinisaili,
Sijui nimwambieni,
Krismasi.
Haupo hausikiki,
Haupo machi,
hadi juni,
Hausikiki julai,
hadi novemba mwishoni,
Mwanangu anisaili,
Utafika lini,
Krismasi?
Mwaka jana ulipokuwa,
tulifurahia ghaya,
Kuku walichinjwa,
sharubati tukanywa,
Chapati na shamrashara,
tukavaa mpya mpya,
Yote tuliyafanya,
ili wewe kukupamba,
Mwanangu anisaili,
Utarejea lini,
Krismasi?
Kutu kuu ya izraili,
Kwa hamu twakusubiri,
Ufike kwetu mastakimuni,
Tuvae vilivyofichika makashani,
Tule vilivyobanzwa makabatini,
Tulie vilivyofukiwa magodoroni,
Tulalapo kitandani,
Tulale si ka' zamani,
Ulipoadimika usingizi,
Na mguso wa mkeangu laini,
Mkeangu anisaili,
Utafika lini,
Krismasi?
Ama wewe mwizi mkuu,
Uliniibia wangu kuku,
Ukaiba bashasha zangu,
Kwa ugomvi na mkeangu,
Alitaka vazi kuntu,
avae katika mashamshamu,
Aliniumiza sana wengu,
Aliponenena, 'acha nende zangu,'
Kwa takwale kulikufuru,
Akinisaili mwanangu,
Nitamhaada kuwa huku,
Hutatia lako guu,
Krismasi!
Ingawa kanihadaa sineni,
karo ya shule sinani,
zafungua mwakani,
Wanangu wa' mgongoni,
Wanidai "baba, nitatiani begini"
Pesa sina sinani,
Sauti yanicheka akilini,
" mpumbavu kalaghaiwa hadharani,
Ulidhani ya siri hatutayabaini! "
Mwangu akinisaili,
Sijui nimwambieni,
Krismasi.
No comments:
Post a Comment