Zungumza,
Siyo kwa kuwa haki unayo,
Ila kwa kuwa ruhasa unayo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una domo,
Ila kwa kuwa una jambo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una maneno,
Ila kwa kuwa una mafunzo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa wajua mengi,
Ila kwa kuwa unafunza wengi,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa imekulazimu,
Ila kwa kuwa umehibu,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una umati,
Ila kwa kuwa una makini,
Zungumza,
Siyo kuwa yule kakushawishi,
Ila kuwa moyo umekushawishi,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una shinikizo,
Ila kwa kuwa una pendeleo,
Zungumza,
Siyo kwa kujiumbua,
Ila kwa kujiumba,
Zungumza,
Siyo kwa kujinaki,
Ila kwa kujitamalaki,
Zungumza,
Siyo kwa kutaka kukasirisha,
Ila kwa kutaka kusuluhisha,
Zungumza,
Siyo kwa kutaka sifa,
Ila kwa kutaka hidaya,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una domo,
Ila kwa kuwa una jambo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa haki unayo,
Ila kwa kuwa ruhasa unayo,
Siyo kwa kuwa haki unayo,
Ila kwa kuwa ruhasa unayo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una domo,
Ila kwa kuwa una jambo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una maneno,
Ila kwa kuwa una mafunzo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa wajua mengi,
Ila kwa kuwa unafunza wengi,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa imekulazimu,
Ila kwa kuwa umehibu,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una umati,
Ila kwa kuwa una makini,
Zungumza,
Siyo kuwa yule kakushawishi,
Ila kuwa moyo umekushawishi,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una shinikizo,
Ila kwa kuwa una pendeleo,
Zungumza,
Siyo kwa kujiumbua,
Ila kwa kujiumba,
Zungumza,
Siyo kwa kujinaki,
Ila kwa kujitamalaki,
Zungumza,
Siyo kwa kutaka kukasirisha,
Ila kwa kutaka kusuluhisha,
Zungumza,
Siyo kwa kutaka sifa,
Ila kwa kutaka hidaya,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa una domo,
Ila kwa kuwa una jambo,
Zungumza,
Siyo kwa kuwa haki unayo,
Ila kwa kuwa ruhasa unayo,
No comments:
Post a Comment