Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Saturday, 3 February 2018

MIMI TIKITI-MAJI

Mcheleni kuna dume,
Tulijua zama zile,
Tulikakanyaga chechele,
Akachaguliwa atekeleze,
Wadhifa wa kilele,
Alijitia umbelembele,
Kwa kauli teletele,
Wakihesabu tunahesabu,
Wakirusha tunarusha,
Wakiapisha tunaapisha,
Muda wetu wa kuapisha,
'Nyumbani nilifungiwa,'
Mimi tikitimaji.

Sauti yangu ilitisha,
Nilipigana kwa ukucha,
Maneno nilisisitiza,
Kanani tutafika,
Magharibi nilitikisa,
Nikisema wanaitikia,
Uwakili ukanisaidia,
Nikapata na useneta,
Kauli nami nilitoa,
Wakihesabu tunahesabu,
Wakirusha tunarusha,
Wakiapisha tunaapisha,
Muda wetu wa kuapisha,
We-tangulia n'takufuata,
Mimi simba mwoga.

Nilikuwa mwasisi wao,
Nikajenga muungano,
Kauli yangu ikawa wimbo,
Nilitamba na NASA HAO,
Magharibi n'kawa mwongozo,
Jina langu likawa Sifo,
Kauli zangu za kiwimbo,
NASA HAOOOOOO!
Wakihesabu tunahesabu,
Wakirusha tunarusha,
Wakiapisha tunaapisha,
Wakati wetu wa kuapisha,
Muda-salia tawe
Mimi ngiri mtu.

No comments:

Post a Comment