Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Wednesday, 28 February 2018

NUNUA VIATU VIWILI

Alikinunua jumatatu,
Hakikuwa na udhaifu,
Kilikuwa sahifu,
Kiling'aa kama dhahabu,
Aendako hakukisahau,
Akilini alikidhukuru,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Iliwadia jumanne,
Akakipaka rangi tele,
Kilichongeka ja mshale,
Alikopita kilipendeze,
Harusi kilimpeleke,
Akakilia na mchele,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Jumatano kaski hiyo,
Kamwe hakuachana nacho,
Alitakiwa kwenye mahojiano,
Atafute kazi ya kipato,
Alikivaa kiatu hicho,
Mwishoni kaona kivuno,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi


Nikwambieje alhamisi,
Alipokaa nyumbani,
Hakukiacha asilani,
Alikitumia bila kujali,
Alikiendea msalani,
Akakanyagia na kinyesi,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Ijumaa kakanyaga bati,
Akielekea msikitini,
Mwanya ukajibuni,
Kwenye ya kiatu soli,
Ndani kikajaa maji,
Alipotembea matopeni,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Jumamosi kwenye soko,
USidhani alikipa kisogo,
Alikikimbilia penye zogo,
Na kukimbia penye sokomoko,
Kiatu kikajaa kokoto,
Soli ikampa mgongo,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Kanisani alilimatia,
Kiatu kilimchubua,
Mguuni aliumia,
Siku nzima alilia,
Hakuwa na cha kutia,
Kiatu chake kiliraruka,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi

Asingekuwa mzulufu,
Aliyejaa upumbavu,
Angevinunua viwili viatu,
Abadilishe kila siku,
Asikitumie kimoja tu,
Kilichompa maumivu,
Heri viwe viwili viatu,
Visaidiane kwenye kazi




3 comments:

  1. Nice one hii inaongelea mini labda yenye nafikiria sio hehe

    ReplyDelete
  2. Vifungu vyenye mnato kweli labda yenye ninafikiria sio tupe uchambuzi wake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nikichambua nitapoteza utamu wake. Uzuri wa fasihi ni kuwa unaifasiri kwa mtazamo wako mwenyewe dada

      Delete