Ukimsikia,
Chura akikoroma,
Wacha kukasirika,
Ati kelele akupigia,
Labda mke atafuta,
Au afurahia mazingira,
Aa pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Simkosoe muumba.
Ukimwona,
Mtoto mchanga,
Alala saaana,
Sione katepetea,
Ndo kwake kujistarehesha,
Na ulimwengu kuusoma,
Au pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Simkosoe muumba.
Ukimfuga Bata
Kila mara aharisha,
Usipange kumuuza,
Kununua asiyeharisha,
Wote ni wamoja,
Mashine yao ndo yasaga,
Changarawe ikasagika,
Halilungi haitamsaidia,
Au pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Simkosoe muumba.
Ukimvua samaki,
Kutoka kwenye maji,
Na mwenye mbaya rihi,
Usimtupe chooni,
Kuwa kaoza ukidhani,
Licha ya kuishi majini,
Hiyo ndo yake rihi,
Au pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Mungu tamkosoa.
Kiwa na jogoo,
Anayewika majogoo,
Na kukatishia ndoto,
Usimpangie kichinjio,
Keleleze kiwa kisingizio,
Au umfunge koo,
Asikwamshe majogoo,
Au pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Mungu tamkosoa.
Tabia kama ngozi,
Kubadilisha huwezani,
Maumbile ya insi
Au zoeacho adinasi,
Usione ni madhambi,
Au pia,
Ni yake mazoea,
Ndivyo alivyoumbwa,
Huwezi ukambadilisha,
Mungu tamkosoa.
@Tungo za Daniel kaka Si'wa

Hongera. Kazi nzuri. Inavutia mno.
ReplyDeleteNimefurahishwa na tungo ili
ReplyDeleteHeko
ReplyDelete