Featured post

KASISI FISADI : LUSAKA AZOMEWA BUNGOMA

 Wanyeji wa Bungoma wamemkemea Gavana wa Jimbo hilo Kenneth Makelo Lusaka. Katika maoni waliyotoa mtandaoni, wananchi wamempaka samli ya ufi...

Sunday, 6 January 2019

SIYATAKI MAPENZI

Sitaki tena kupenda
Ninakimbia nanenda
Nimeshindwa udifenda
Sivumilii ninakwenda

Mapenzi yamenisibu
Ndwele iso matibabu
Menisaliti muhibu
Amerarua kitabu

Kwa hali lijitolea
Makubwa kamtendea
Mabaya meninenea
Nakwenda natokomea

Majonzi linizidia
Usiku lijililia
Penzi lochangamkia
Kwa sasa lanichukia

Mwenyezi nihurumie
Machungu nipunguzie
Siniache nijililie
Nishike sijifilie

5 comments: