Sitaki tena kupenda
Ninakimbia nanenda
Nimeshindwa udifenda
Sivumilii ninakwenda
Mapenzi yamenisibu
Ndwele iso matibabu
Menisaliti muhibu
Amerarua kitabu
Kwa hali lijitolea
Makubwa kamtendea
Mabaya meninenea
Nakwenda natokomea
Majonzi linizidia
Usiku lijililia
Penzi lochangamkia
Kwa sasa lanichukia
Mwenyezi nihurumie
Machungu nipunguzie
Siniache nijililie
Nishike sijifilie
Ninakimbia nanenda
Nimeshindwa udifenda
Sivumilii ninakwenda
Mapenzi yamenisibu
Ndwele iso matibabu
Menisaliti muhibu
Amerarua kitabu
Kwa hali lijitolea
Makubwa kamtendea
Mabaya meninenea
Nakwenda natokomea
Majonzi linizidia
Usiku lijililia
Penzi lochangamkia
Kwa sasa lanichukia
Mwenyezi nihurumie
Machungu nipunguzie
Siniache nijililie
Nishike sijifilie
Kipawa unacho kaka! Kitumie vilivye! Mola aibariki kazi yako. Hongera!
ReplyDeleteKaka Webi.
Kitumie kipawa vilivyo!
ReplyDeleteHeko kwako Kaka Naona kweli kipaji unacho kitumie sawasawa
ReplyDeleteGreat
ReplyDeleteKazi kuntu
ReplyDelete